Simba Yapasuka Dabi ya Kariakoo

Klabu ya Simba imeshindwa kufurukuta hapo jana kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo baada ya kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga mchezo ambao ulipigwa majira ya saa 1:00 usiku katika dimba la Benjamin Mkapa.

Simba Yapasuka Dabi ya Kariakoo

Mchezo huo ulikuwa ni Ngao ya Jamii ambao ulikuwa ni nusu fainali ya pili, huku bao hilo likitupiwa katika dakika 45 za kipindi cha kwanza na Max Nzengeli na hilo ndilo lililosalia mpaka mwisho wa mchezo.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Mchezo ulikuwa ni wa kuvutia sana kwani timu zote zilikuwa zikihitaji ushindi kwa hali na mali huku Simba akiwa na kazi ya kufanya kujiandaa na msimu ujao kwani timu yao takribani yote ni mpya hivyo mashabiki wanahitaji uvumilivu wakati timu ikijipanga.

Simba Yapasuka Dabi ya Kariakoo

Baada ya Yanga chini ya kocha mkuu Miguel Gamondi kushinda, hivyo basi mchezo wa fainali watacheza dhidi ya Azam FC ambao wao walishinda 5-2 dhidi ya Coastal Union mchezo ambao ulipigwa kule visiwani Zanzibar.

Baadhi ya mashabiki ambao Meridian Sport walifanya nao mahojiano wameikubali timu yao na kuwapongeza wachezaji kwa kiwango ambacho wamekionyesha na kusema kuwa hawawadai kitu kwani timu bado ni mpya wakipange kwenye ligi tuu.

Simba Yapasuka Dabi ya Kariakoo

Fainali ya Ngao ya Jamii itapigwa siku ya Jumapili kati ya Azam FC dhidi ya Yanga katika dimba la Benjamin Mkapa, wakati mshindi wa tatu kati ya Simba dhidi ya Coastal Union majira ya saa nane mchana.

Acha ujumbe