Klabu ya Simba imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya Afrika baada ya kushinda mchezo wake wa hatua ya awali wa ligi ya mabingwa barani Afrika.

Wekunda wa msimbazi wanafanikiwa kwenda hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kushinda michezo miwili ya hatua ya awali dhidi ya Nyasa Big Bullets kwa jumla ya mabao manne kwa bila.

simbaSimba walifanikiwa kupata ushindi wa magoli mawili kwa bila katika mchezo wa awali waliocheza ugenini nchini Malawi kupiitia magoli ya Moses Phiri na John Bocco kabla ya kukamilisha ushindi huo siku ya leo katika dimba la Benjamin Mkapa baada ya kushinda mabao mawili kwa bila huku Moses Phiri akiwa ametakata baada ya kufunga mabao yote mawili katika mchezo huo.

Mnyama atasubiri mshindi kati ya Primero de Agosto dhidi ya Red Arrows katika mchezo wa hatua ya pili ya michuano hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa