Simeone Inzaghi kocha wa klabu ya Inter Milan amepanga kupata alama kumi katika kundi C ambapo kuna vilabu vya Barcelona,Bayern, na klabu ya Victoria Plzen ya nchini ya Jamhuri ya Czech.

Katika ambalo linaonekana kua gumu sana kocha huyo anafikiri angalau kupata alama kumi itawasaidia wababe hao wa soka kutoka nchini Italia ili kuweza kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

simeoneInter Milan wanapanga kuvuna alama nyingi zaidi kutoka katika klabu ya Victoria Plzen ya nchi ya Jamhuri ya Czech ambao ndo wanaonekana ndio timu isiyotisha kwenye kundi hilo.

Inter ambao wamepoteza mchezo wa awali dhidi ya klabu ya Fc Bayern Munich kwa goli mbili kwa bila amabao unakua mchezo wao wa pili kupoteza katika mchezo wa ufunguzi mara ya mwisho ulikua msimu wa 2006/07 chini ya mwalimu Roberto Mancini hivo wanatazamia mchezo wa leo dhidi ya Victoria Plzen kupata matokeo ili kujiweka katika mazingira magumu.

Inzaghi anasema wanahitaji kurudisha utimamu baada ya kupoteza mchezo wa awali huku akilitaja kundi lao kama kundi gumu zaidi.

“Bila shaka,ni mchezo muhimu na tupo kwenye kundi gumu zaidi kwenye ligi ya mabingwa lakini tumejiandaa kucheza”Inzaghi aliwaambia waandishi wa habari jumatatu.

“Mchezo wa kwanza haukua bora kwetu sisi, Bayern walikua bora kuliko sisi na tunajiandaa kwenda kucheza mchezo ambao uanaweza kutuweka hatarini zaidi lakini tumejipanga kwa njia bora zaidi” alieleza Simeone kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Victoria Plzen.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa