Kocha Msaidizi wa Singida Big Stars Mathias Lule, amesema kuwa wachezaji wote ambao wapo ndani ya kikosi hicho watapata nafasi ya kucheza na kuonyesha uwezo wao na ni jukumu lao kujituma kila watakapokuwa wanapewa nafasi hiyo.

Singida Big Stars kwa sasa inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Septemba 21.

Singida Big Stars, Singida Big Stars Wapewa Matumaini Mapya, Meridianbet

Miongoni mwa mastaa ambao wapo ndani ya kikosi hicho ni pamoja na Amis Tambwe, Meddie Kagere, Aziz Andambwile, Pascal Wawa ambaye ni nahodha wa kikosi hicho.
“Hakuna mchezaji ambaye anapenda kuanza benchi lakini hilo lipo kwenye maamuzi ya benchi hivyo wale wanaopata nafasi wanacheza kwa kushirikiana na wale ambao wataanza.

“Ni suala la muda tu kila mchezaji atapata nafasi ya kucheza kwani kila aliyepo hapa anastahili kucheza ndio maana akasajiliwa kikubwa kwao ni kuonyesha jitihada,” amesema.
Kwenye msimamo Singida Big Stars imekusanya pointi 7 baada ya kucheza mechi tatu ikiwa nafasi ya tano.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa