Mpira wa Miguu, Soka wazungu wanaita Football ulianza kuchezwa mwanzoni mwa karne ya 19 na kwa kipindi hiko radha ya soka ilikua ni kutazama matukio halisi na kuongeza mvuto wa kwenye mchezo husika, Kama utakumbuka mwezi Juni 22 1986 Diego Maradona alifunga goli kwa mkono lililoperekea Argentina kuibuka na ushindi wa goli 2-1 Dhidi ya Uingereza na kuvuka hatua ya robo fainali ya kombe la dunia kwa mwaka huo.

Soka

Leo hii tunashuhuda mapiduzi ya kiteknolojia katika soka la ulimwengu katika mifumo mbali mbali inayoendelea kuboreshwa chini ya taasisi zinazo simamia mpira wa miguu duniani na kwenye nataifa husika.

Hivi karibuni ilitambuliswa ulimwenguni teknolojia ya Goal Line Technology ambayo ililenga kusaidia vituambavyo havingeweza kuonekana kwa jicho la kawaida kwa waamuzi. Wakati ina Anzishwa wapenda michezo wengi wamekua waki ibeza teknolojia hii kwakua ilikua na mapungufu kadha wakati inatambuliswa kwenye soka la kisasa.

Imekua kawaida sana kwa sasa kuona Goli lililo andaliwa kiufundi na mpangilio mzuri wa ki timu kukataliwa kwa sababu za ki teknolojia, Mara nyingine inapunguza hali ya mchezo hususan kwa wachezaji wanao shiriki mchezo husika, lakini pia ile radha ya soka kwa mashabiki imekua inapungua siku hadi siku kutokana na kuwepo kwa teknolojia katika mchezo ambao maamuzi yake yalizingatia zaidi maamuzi ya muamuzi wa kati.

Soka

Tafakari hii, Wakati mpira unaanzishwa kati na timu A kuelekea timu B mchezaji wa timu B alifanyiwa madhambi lakini muamuzi hakuona na wachezaji wa timu A waliendelea na shambulizi na wakati huo huo hawa wa timu B walijitahidi kuzuia. Goli linapopatikana kwenye mchezo wa namna hii maamuzi yanaweza kuvurugwa na goli kufutwa na kupoteza ile radha halisi ya mchezo.

Wakati huo huo wapo wanaoifurahia teknolojia kwenye mchezo wa soka kwa kua kwa namna moja au nyingine imekuja kuleta usawa na haki kwenye maamuzi ya michezo husika, Ule utaratibu wa timu kutoka kwenye mashindano kwa sababu imefungwa goli la Offside, Goli la mkono au aina yoyote ya matukio ambayo yanakinzana na haki.

Mwisho kabisa niliache swali kwa wapenda michezo kua kipi ni sahihi kuacha teknolojia iuendeshe mpira au tuachane mpira uendeshwe kama zamani.?


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

soka, Soka :Teknolojia Inaharibu au Kuongeza Radha Kwenye Soka?, Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa