Klabu ya Southampton haijalala wakati nwa dirisha la usajili majira haya ya kiangazi sasa wamekamilisha usajili wa kumsaini golikipa Gavin Bazunu kutoka Manchester City kwa dau linaloripotiwa kuwa pauni milioni 12.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland ameicheza michezo 10 nchi yake lakini hajawahi kuichezea Man City tangu asajiliwe mwaka 2019 akitokea Shamrock Rover kwa dili ya mika mitano.

Baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu uliyoisha kwa kumaliza katia nafasi ya 15 Southampton inataka kukiimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao 2022-23 na usajili wa Bazunu utakuwa unamanufaa sababu Fraser Froster anatimkia Tottenham mwisho wa mwezi huu baada ya kumaliza mkataba wake na Saints.

Kocha wa Southampton Hasenhuttl amesema uzoefu wa Bazunu wa kufanya kazi na vijana wa Pep Guardiola unamfanya kuwa mchezaji bora.

“Ni kipa mwenye uchezaji wa kisasa sana, anayejiachia katika hatua ya maandalizi, ambaye ameimarika kimwili kupitia uhamisho wa mkopo muhimu mapema katika kazi yake,” alisema.

“Tayari ni kipa wa kimataifa, jambo ambalo ni nadra sana kwa umri wake.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa