Szczesny Aukubali Ukweli Kushuka Kiwango Chake

Kipa mkongwe Wojciech Szczesny ameonyesha ukomavu mkubwa baada ya kukiri wazi kuwa hana tena kiwango kile cha juu alichokuwa nacho miaka ya nyuma, huku akimuunga mkono Joan García kuendelea kuwa chaguo la kwanza langoni mwa Barcelona.

Szczesny Aukubali Ukweli Kushuka Kiwango Chake

Licha ya taarifa kuwa alikataa ofa kutoka klabu nyingine kubwa La Liga ili kuendelea kubaki Camp Nou hadi mkataba wake umalizike mwaka 2027, Szczesny ameonekana kukubaliana na nafasi yake mpya ndani ya kikosi. Kwa sasa, kipa huyo wa Poland anatumika zaidi kama mbadala wa Joan García ambaye ameendelea kuaminiwa zaidi na benchi la ufundi.

Katika mechi zake 10 akiwa Barcelona, Szczesny ameruhusu mabao 17 lakini bado anaendelea kuwa sehemu muhimu ya timu kutokana na uzoefu wake mkubwa. Hata hivyo, mwenyewe amesema wazi kuwa sasa anaelewa kuna makipa wenye kiwango bora zaidi yake kwa wakati huu wa soka la kisasa.

Szczesny Aukubali Ukweli Kushuka Kiwango Chake

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kauli yake ya kumuunga mkono Joan García imewavutia mashabiki wengi wa Barcelona, wakiona ni ishara ya heshima na uongozi mzuri ndani ya timu. Szczesny amesema anafurahia kumuona kipa huyo mdogo akiendelea kukua na hana tatizo kumuunga mkono kwa kila hatua.

Szczesny Aukubali Ukweli Kushuka Kiwango Chake

Ripoti zinaeleza kuwa kipa huyo mwenye miaka 36 sasa anaangalia zaidi furaha ya maisha na familia kuliko pesa au muda mwingi wa kucheza. Ndiyo maana anaonekana kufurahia maisha nchini Hispania badala ya kukimbilia ligi kama MLS au Saudi Arabia, huku akijiandaa taratibu kuelekea mwisho wa safari yake ya soka.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.