Szoboszilai Aomba Radhi kwa Mashabiki Wa Liverpool Baada ya Kutoelewana

Kiungo wa Liverpool FC, Dominik Szoboszlai, ameomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo kufuatia tukio lililotafsiriwa vibaya kuhusu lugha yake ya mwili baada ya kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Manchester City katika robo fainali ya FA Cup.

Szoboszilai Aomba Radhi kwa Mashabiki Wa Liverpool Baada ya KutoelewanaWachezaji wa Liverpool walizomewa walipokwenda kuwashukuru mashabiki wao baada ya kipigo hicho kikubwa, huku Szoboszlai akionekana kuinua mabega, kupiga makofi na kuonyesha ishara zilizotafsiriwa na wengi kama dhihaka au kukasirishwa na mashabiki.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika tukio hilo, Szoboszlai aliondolewa haraka na mwenzake Federico Chiesa, lakini baadaye alijitokeza hadharani kuelezea kilichotokea na kusisitiza kuwa hakumaanisha ubaya wowote.

Szoboszilai Aomba Radhi kwa Mashabiki Wa Liverpool Baada ya Kutoelewana“Labda kulikuwa na kutoelewana kati yangu na mashabiki. Sikumaanisha kwa njia mbaya. Najua mashabiki wana maana kubwa kwa klabu hii na klabu ina maana kubwa kwao,” alisema Szoboszlai.

Aliongeza kuwa wachezaji wanafanya kila kitu kwa ajili ya mashabiki, na endapo ishara zake zilieleweka vibaya, basi anaomba radhi. “Hatupo juu yao, tunahisi sawa kabisa kama wanavyohisi. Tuko pamoja nao, na tunatarajia wao pia wawe pamoja nasi,” alisisitiza.

Szoboszilai Aomba Radhi kwa Mashabiki Wa Liverpool Baada ya KutoelewanaWakati huo huo, Liverpool wanakabiliwa na hatari ya kutolewa katika UEFA Champions League na Paris Saint-Germain, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza jijini Paris. Szoboszlai amesema wako tayari kupambana hadi mwisho katika mchezo wa marudiano. “Tutapambana kwa nguvu zote na kutoa kila tulicho nacho. Niko tayari kufa uwanjani. Kila kitu kinawezekana Anfield,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.