UWANJA wa Mkapa mchezo wa kuwania kufuzu CHAN, timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars imefanikiwa kuibuka na ushindi mbele ya Somalia.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Somalia 0-1 Tanzania na kuwafanya Watanzania kuweza kuanza kwa ushindi kwenye mchezo wa leo.

Tanzania, Tanzania Yajisafishia Njia ya Kwenda CHAN, Meridianbet

Mtupiaji wa bao la Tanzania ni kiungo Abdul Suleiman, ‘Sopu’ ambaye alipachika bao hilo dk 46 kwa maji yaliyomwaga na Kibwana Shomari.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza ziliyeyuka kwa timu zote kushindwa kufungana katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo ujao Tanzania itakuwa nyumbani unatarajiwa kuchezwa Julai 30 na mshindi wa jumla anatarajiwa kumenyana na timu ya taifa ya Uganda.

Kipa ambaye alianza kikosi cha kwanza Aishi Manula alipata maumivu dk 87 na nafasi yake iliweza kuchukuliwa na Mshery Aboutwalib.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa