Tanzania Yaanza Vibaya Michuano ya AFCON

Michuano ya AFCON barani Afrika inazidi kupamba moto huko Morocco ambapo timu kadhaa zimeanza vyema na zingine zikianza vibaya ikiwemo Tanzania ambapo walipigika kwa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria mechi iliyopigwa katika dimba la Fez mjini Fez nchini Morocco.

Tanzania Yaanza Vibaya Michuano ya AFCON

Mabao ya Super Eagles yamefungwa na beki wa Hull City ya England, Oluwasemilogo Adesewo Ibidapo “Semi” Ajayi dakika ya 36 na winga wa Atalanta ya Italia, Ademola Lookman Olajade Alade Ayoola Lookman dakika ya 52, wakati la Taifa Stars limefungwa na kiungo wa Floriana ya Malta, Kokola Charles William M’Mombwa dakika ya 50.

Kipigo hicho ni mwendelezo wa ubabe wa Nigeria kwa Tanzania kwenye Fainali za AFCON na mashindano yote kwa ujumla.

Mara ya kwanza timu hizo kukutana kwenye Fainali za AFCON ilikuwa ni mwaka 1980 na Nigeria wakiwa wenyeji waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 Machi 8 Uwanja wa Surulere Jijini Lagos.

Zaidi ya hapo timu hizo zimekutana mara mbili katika mechi za Kundi G kufuzu AFCON ya 2017, Super Eagles ikiendeleza ubabe kwa ushindi wa 1-0 nyumbani Septemba 3 mwaka 2016 bao la Kelechi Iheanacho dakika ya 79 wakati huo akitokea Manchester City na huo ulikuwa mchezo wa marudiano baada ya taifa Stars kulazimishwa suluhu (0-0) Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Septemba 5, mwaka 2015.

Tanzania Yaanza Vibaya Michuano ya AFCON

Kwa ujumla Tanzania haijawahi kushinda mechi hata katika Fainali zote tatu za awali za AFCON ilizocheza; Mwaka 1980 walifungwa 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri pamoja na Sara ya 1-1 na Ivory Coast, 2019 walifungwa mechi zote, 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria — wakati mwaka 2023 walifungwa mechi moja, 3-0 na Morocco na sare za 1-1 na Zambia na 0-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.