Serikali ya Tanzania imechukua hatua kubwa katika maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 kwa kutenga dola milioni 30, sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 76. Uwekezaji huo ukiwa na dhamira ya nchi kuhakikisha mashindano hayo makubwa barani Afrika yanafanyika kwa viwango vya juu na vinavyokubalika kimataifa.

Akizungumza bungeni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika kama ada ya uandaaji na sehemu ya maandalizi ya miundombinu muhimu. Alisisitiza kuwa Tanzania, pamoja na washirika wake, imejipanga kuhakikisha AFCON 2027 inakuwa ya kipekee na ya kihistoria.
Serikali pia imeweka mkazo katika kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo viwanja vya michezo, barabara na huduma za hoteli. Ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na ujenzi wa viwanja vipya vya mazoezi unatajwa kuwa sehemu muhimu ya maandalizi hayo yanayoendelea kwa kasi nchini.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Makonda alikumbusha pia mafanikio ya Tanzania katika CHAN 2024, ambapo taifa liliandaa mashindano hayo kwa mafanikio makubwa na Taifa Stars kufika robo fainali. Alisema uzoefu huo umeongeza ujasiri na kuonyesha kuwa Tanzania inaweza kuandaa mashindano ya kiwango cha kimataifa bila changamoto kubwa.

Kwa ujumla, uwekezaji huu mkubwa unaashiria Tanzania kujikita zaidi katika michezo kama sekta ya kiuchumi na utalii. Serikali inaamini kuwa AFCON 2027 haitakuwa tu mashindano ya soka, bali pia fursa ya kuonyesha uwezo wa nchi, kuvutia wageni na kukuza uchumi kupitia michezo.


