Marc Ander ter Stegen golikipa wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Ujerumani aongoza katika orodha ya makipa walioruhusu mabao machache katika ligi bora tano ulaya.

Golikipa huyo raia wa Ujerumani ameongoza kwa kumaliza michezo kwa kutokuruhusu mabao huku akiwa na michezo mitano akiwa hajaruhusu wavu wake kuguswa kabisa akifyatiwa na golikipa wa Freiburg Mark Flekken inayoshiriki ligi kuu ujerumani ambae ana michezo mitano na yeye huku ikiisaidia timu yake kuongoza ligi kuu ya Ujerumani,Gigi Donnarumma kutoka PSG akiwa ana michezo mitano pia,Ederson wa klabu ya Man City akiwa na michezo minne huku Geromino Rulli nae akiwa na michezo minne.

ter stegenKinachomtofautisha Ter Stegen na wenzake waliofungana michezo mitano ni kua golikipa huyo hajaruhusu bao katika michezo mitano huku akiwa ameruhusu bao moja tu katika michezo aliyocheza msimu huu katika ligi kuu nchini Hispania.

Stegen amekua na kiwango bora sana kwenye miamba hiyo ya Catalan tangu ajiunge klabuni hapo mwaka 2014 hata pale timu hiyo inapokua haifanyi vizuri amekua msaada mkubwa kwa klabu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa