Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Paris St-Germain imempatia mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, kitita cha euro milioni 150 kwa misimu miwili ili abaki klabuni hapo.

Tetesi zinasema, Manchester United imetuma mawakala kumuangalia winga wa Villarreal Arnaut Danjuma akicheza dhidi ya Bayern Munich. Winga huyo pia anawindwa na Liverpool.

Tetesi zinasema, Brazil inajiandaa kumpatia meneja wa Manchester City Pep Guardiola donge nono ili awe kocha wa timu yao ya taifa.

Bosi wa Everton, Frank Lampard anaungwa mkono na mmiliki wa klabu Farhad Moshiri na bodi ya klabu ya Goodison Park, licha ya Toffees kukaa pointi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja la Ligi Kuu.

Newcastle na West Ham wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Union Berlin na Nigeria striker Taiwo Awoniyi, 24, msimu huu wa majira ya joto.

Wolves wamemuona kiongo wa kati wa Sporting Lisbon na Portugal Joao Palhinha, 26, kuwa anafaa ikiwa Ruben Neves akaondoka msimu huu wa majira ya joto.

Tetesi zinasema, Manchester United inajiandaa kuvunja rekodi yake katika usajili na kumsajili kiongo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 23.

Arsenal, Manchester United na Tottenham wameambiwa kuwa watahitajika kulipa £67m ikiwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 22, kutoka klabu ya huko Portugal Benfica.

Leeds United na Brighton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 22.

Tetesi zinasema, Spurs wamekubali kumsajili kiungo wa kati wa Brentford na Denmark Christian Eriksen, 30, kurudi klabuni hapo.

Meneja wa Newcastle Eddie Howe anasema kuwa winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin (25) anaweza kusalia klabuni hapo mbali ya kuwa na tetesi za kuondoka.

Newcastle pia wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 28.

 

Paulo-Dybala

Mshambuliaji wa Fulham na timu ya taifa ya Portugal chini ya miaka 21 (U21) Fabio Carvalho, 19, amekuali kuhamia Liverpool.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Uruguay striker Luis Suarez, 35, yupo kwenye mazungumzo na klabu za Uturuki Fenerbahce na Besiktas.

Mshamuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, anataka mkataba wa miaka mitatu kama atajiunga na Barcelona msimu huu wa majira ya joto.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe