TFF Yachukua Hatua Kali Dhidi ya Utovu wa Nidhamu NBC Premier League

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limetangaza adhabu mbalimbali kwa klabu na wachezaji wa NBC Premier League kutokana na matukio ya utovu wa nidhamu yaliyotokea katika michezo tofauti msimu huu.

TFF Yachukua Hatua Kali Dhidi ya Utovu wa Nidhamu NBC Premier LeagueMchezaji wa Yanga SC, Mudathir Yahya, amefungiwa michezo mitatu pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 1 baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji FC, Ibrahim Abraham, wakati wa mchezo uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika mechi nyingine namba 146, klabu ya Coastal Union FC imetozwa faini ya Shilingi milioni 5 baada ya mashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani wakati wa vurugu zilizohusisha mwamuzi wa kati na mwamuzi msaidizi, kufuatia tukio kati ya mchezaji wa Mtibwa Sugar FC, Victor Collins, na Athuman Makambo.

TFF Yachukua Hatua Kali Dhidi ya Utovu wa Nidhamu NBC Premier LeagueKatika mechi namba 151, klabu ya Singida BS pia imepigwa faini ya Shilingi milioni 5 baada ya viongozi wake wawili kuingia uwanjani na kumwaga vimiminika, tukio lililotafsiriwa kama vitendo vinavyohusishwa na imani za kishirikina kabla ya maandalizi ya mchezo dhidi ya TRA United.

TFF Yachukua Hatua Kali Dhidi ya Utovu wa Nidhamu NBC Premier LeagueKwa upande mwingine, klabu ya Azam FC imetozwa faini ya Shilingi milioni 5 baada ya viongozi wa benchi la ufundi na wachezaji kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani kinyume na kanuni za mchezo na makubaliano ya kikao cha maandalizi ya mechi.

TFF Yachukua Hatua Kali Dhidi ya Utovu wa Nidhamu NBC Premier LeagueTFF imesisitiza kuwa adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu, hasa Kanuni ya 47:1 na Kanuni ya 17:62, ikilenga kudumisha nidhamu, heshima na usalama ndani ya viwanja vya mpira nchini.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.