TFF Yatupilia Mbali Malalamiko ya Simba Kuhusu Usajili wa Damaro Camara

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limetoa uamuzi rasmi kuhusu sakata la uhalali wa usajili wa mchezaji Mohamed Damaro Camara, likibainisha kuwa hakuna ukiukwaji wa kanuni uliofanyika kama ilivyodaiwa na klabu ya Simba.

TFF Yatupilia Mbali Malalamiko ya Simba Kuhusu Usajili wa Damaro CamaraUamuzi huo umetolewa baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuchambua kwa kina malalamiko yaliyowasilishwa na Simba, waliokuwa wakipinga usajili huo wakidai mchezaji huyo alicheza mechi 13 badala ya 12 zinazoruhusiwa kikanuni.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, kamati hiyo ilichunguza Kanuni ya 6.2(1) ya Ligi Kuu pamoja na miongozo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kabla ya kufikia hitimisho lake.

TFF Yatupilia Mbali Malalamiko ya Simba Kuhusu Usajili wa Damaro CamaraKamati imejiridhisha kuwa usajili wa Camara uko sahihi na haukiuki kanuni zozote za soka,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya TFF.

Aidha, TFF imeeleza kuwa uamuzi huo ni wa mwisho kwa hatua ya awali, huku ikibainisha kuwa Simba wana haki ya kukata rufaa iwapo hawajaridhika na maamuzi hayo.

TFF Yatupilia Mbali Malalamiko ya Simba Kuhusu Usajili wa Damaro CamaraHatua hiyo inatarajiwa kupunguza mjadala uliokuwa umeibuka miongoni mwa wadau wa soka nchini, wakati mashabiki na klabu wakisubiri kuona kama Simba watachukua hatua ya kukata rufaa au kukubaliana na uamuzi huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.