Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, limetangaza kuufungia rasmi Uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma kwa matumizi ya michezo ya Ligi kufuatia kushindwa kukidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Machi 22, 2026, TFF imeeleza kuwa miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa yaliyowekwa chini ya Kanuni za Leseni za Klabu, hali inayolazimu kuchukuliwa kwa hatua hiyo ili kulinda ubora na usalama wa mashindano.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kutokana na uamuzi huo, timu zote zinazotumia Uwanja wa Jamhuri kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutafuta viwanja mbadala kwa muda, hadi pale maboresho yatakapofanyika na kukaguliwa upya na TFF.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa kufunguliwa tena kwa uwanja huo kutategemea kukamilika kwa marekebisho ya miundombinu pamoja na kupitishwa rasmi na mamlaka husika ndani ya TFF.
Aidha, TFF imezikumbusha klabu zote nchini kuendelea kuzingatia na kuboresha miundombinu ya viwanja vyao ili kuendana na matakwa ya kanuni, hatua inayolenga kuimarisha kiwango cha soka la Tanzania pamoja na ushindani wa ligi zake.

