“The King is Back”: Salah Aanza Mazoezi, Misri Kuwakabili Australia

Nahodha wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, amerudi mazoezini siku ya Jumanne akiwa sehemu ya kikao cha mazoezi ya timu hiyo, hatua inayoongeza matumaini ya kupona kwake kabla ya mchezo wa hatua ya 32 Bora wa michuano ya Dunia dhidi ya Australia utakaochezwa Ijumaa.

“The King is Back”: Salah Aanza Mazoezi, Misri Kuwakabili Australia Salah alikuwa akipata matibabu baada ya kupata maumivu ya nyama za paja (hamstring) na alilazimika kutolewa uwanjani katika mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Iran katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi, hali iliyozua wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kushiriki mechi ijayo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Picha zilizosambazwa kupitia ukurasa wa Shirikisho la Soka la Misri kwenye Facebook zilimuonesha Salah akiwa anatabasamu na akiwa tena uwanjani akifanya mazoezi na wenzake katika mji wa Spokane, ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Australia.

“The King is Back”: Salah Aanza Mazoezi, Misri Kuwakabili Australia Katika ujumbe wao, timu ya taifa ya Misri iliandika “The King is back”, kauli iliyopokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki huku ikiongeza morali ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi lao kwa pointi tano.

“The King is Back”: Salah Aanza Mazoezi, Misri Kuwakabili Australia Salah, mwenye umri wa miaka 34, amekuwa mhimili muhimu wa safari ya Misri katika mashindano hayo, akifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao, huku kurejea kwake mazoezini kukionekana kama ongezeko kubwa la nguvu kuelekea mchezo muhimu wa Ijumaa dhidi ya Australia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.