Kocha wa Senegal, Pape Thiaw, amesema kikosi chake kiko tayari kuanza upya safari ya michuano Dunia dhidi ya Ubelgiji katika hatua ya 32 Bora itakayochezwa Jumatano mjini Seattle, akisisitiza kuwa matokeo ya hatua ya makundi yamewekwa kando.
Senegal ilifanikiwa kusonga mbele kama moja ya timu zilizofuzu kwa nafasi ya tatu, licha ya kupoteza mechi mbili dhidi ya Ufaransa na Norway. Hata hivyo, ushindi mkubwa wa mabao 5-0 dhidi ya Iraq uliwawezesha kufuzu kutokana na tofauti bora ya mabao, katika kundi lililokuwa na ushindani mkali.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo, Thiaw alisema: “Tuna heshima kubwa kwa Ubelgiji, ni taifa kubwa la soka na limeonyesha ubora wake. Tuko tayari, tumejiandaa.” Aliongeza kuwa: “Tunalijua Ubelgiji walikuwa vinara wa kundi lao, lakini sisi tumepigana kufika hapa. Tulilazimika kupambana kwa nguvu, na sasa ni mashindano mapya kabisa, tunahitaji ushindi.”
Kikosi cha Senegal kinakumbwa na pengo la golikipa wake namba moja, Edouard Mendy, ambaye alikosa mchezo uliopita dhidi ya Iraq kutokana na majeraha. Hata hivyo, Thiaw amethibitisha kuwa mchezaji huyo ataungana na timu nchini Marekani baada ya safari ya kurudi klabu yake ya Al Ahli kwa matibabu, huku akitarajiwa kurejea kikosini muda wowote.
Senegal ni miongoni mwa mataifa tisa ya Afrika yaliyofuzu hatua ya mtoano, rekodi mpya kwa bara hilo kutokana na ongezeko la timu katika mashindano. Ushindi dhidi ya Ubelgiji utakuwa wa kihistoria kwa Senegal kwani utaweka kikomo cha miaka 24 bila mafanikio makubwa katika hatua ya mtoano ya mashindano ya Dunia.


