Kocha wa Senegal, Pape Bouna Thiaw, amesema matumaini ya timu yake kufuzu hatua inayofuata ya mashindano ya Dunia 2026 bado yapo hai licha ya kupokea kichapo cha pili mfululizo, safari hii wakifungwa mabao 3-2 na Norway katika mchezo wa Kundi I uliochezwa Jumatatu.
Senegal, ambayo ilianza mashindano kwa kupoteza mabao 3-1 dhidi ya Ufaransa, sasa ipo katika mazingira magumu ya kufuzu. Hata hivyo, Thiaw amesisitiza kuwa kikosi chake hakitakata tamaa na kitaendelea kupigania nafasi ya kusonga mbele kupitia orodha ya timu bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Ulikuwa mchezo mgumu dhidi ya Norway, timu yenye ubora mkubwa ambayo ilitupa changamoto nyingi. Tuliruhusu mabao katika nyakati mbaya sana, moja kabla ya mapumziko na lingine mara tu baada ya kuanza kipindi cha pili. Tunapaswa kuwapongeza Norway kwa ushindi wao,” alisema Thiaw.
Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kutovunjika moyo kutokana na matokeo hayo, akisisitiza kuwa walipambana kwa lengo la kupata pointi tatu lakini mambo hayakwenda kama walivyotarajia. “Ninawahimiza wachezaji wangu wasikate tamaa. Tulitaka kuondoka na ushindi, lakini haikuwezekana usiku huu. Hata hivyo, bado hatujashindwa kabisa,” aliongeza.

Senegal sasa italazimika kuifunga Iraq katika mchezo wake wa mwisho wa makundi utakaochezwa Toronto ili kubaki na matumaini ya kufuzu. “Bado tuna mchezo mmoja mbele yetu. Tunahitaji kuuelekeza nguvu zote huko, kupata pointi tatu na kusubiri matokeo mengine. Hatuko katika nafasi nzuri, lakini bado tupo hai kwenye mashindano. Tukifanikiwa kufuzu, itakuwa kama mashindano mapya yanaanza,” alihitimisha Thiaw.


