Thomas Partey ameingia kwenye orodha ya wachezaji majeruhi kwenye klabu ya Arsenal na anatarijia kukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Brighton kutokana na majeruhi aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace siku ya jumatatu ambapo walipoteza kwa goli 3-0.
Ukimuondoa Thomas Partey, wachezaji wengine wa Arsenal ambao wamethibitishwa na kocha Mikel Arteta mapema wiki hii kuwa majeruhi, ni Kieran Tierney ambaye ana majeraha ya goti ambayo yatamuweka nje ya msimu na Takehiro Tomiyasu ambaye bado anatatizo la mguu.

Arsenal wamesema Partey, tatizo lake la nyoga ya kulia alilolipta kwenye mchezo dhidi ya Palace ni endelevu, na inaonekana kuwa atakosa mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Southampton na Chelsea pia.
“Mchezaji wetu namba tano ambaye alitolewa kwenye mchezo wa jumatatu dhidi ya Crystal Palace kwenye dimba la Selhurst Park, baada ya kupata tatizo la nyonga ya kulia, amekuwa akifanyiwa vipimo na imeoneka kuwa anatatizo kwenye nyonga yake ya kuria.
Tutaendelea kumfanyia vipimo zaidi kwa wiki zijazo, na Kwa lipindi ambacho atakuwa nje pia atapa msaada wa ushauri wa madaktari bingwa. Na kila mmoja atafanya kazi kwa kujudi ili kuhakisha Thomas Partey anarejea haraka iwezekanavyo.” Waraka wa klabu ya Arsenal.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.