Tottenham Yakamilisha Usajili wa Savinho Kutoka Manchester United kwa £75M

Tottenham Hotspur imekamilisha usajili wa winga wa Brazil, Savinho, kutoka Manchester City kwa ada ya awali ya pauni milioni 75, ambayo inaweza kufikia pauni milioni 85 iwapo vigezo vya nyongeza vitatimia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye sasa anatumia jina Sávio, amesaini mkataba wa muda mrefu na Spurs.

Tottenham Yakamilisha Usajili wa Savinho Kutoka Manchester United kwa £75MKocha wa Tottenham, Roberto De Zerbi, amemkaribisha Sávio akiamini kuwa atakuwa nyongeza muhimu katika kikosi chake. “Sávio anaongeza nguvu, ubunifu na uwezo wa kuwachanganya mabeki katika maeneo ya pembeni,” alisema De Zerbi, huku akitarajia mchezaji huyo kusaidia kuongeza kasi na ubunifu katika safu ya ushambuliaji ya Spurs.

Sávio alicheza jumla ya mechi 24 za Premier League msimu uliopita akiwa Manchester City, akianza michezo saba. Kwa ujumla, alicheza mechi 84 akiwa na City na kufunga mabao saba, kabla ya kuamua kuhamia Tottenham katika dili ambalo linaweza kuwa moja ya mauzo makubwa zaidi katika historia ya Manchester City.

Tottenham Yakamilisha Usajili wa Savinho Kutoka Manchester United kwa £75MUsajili huo umeifanya Tottenham kuvuka zaidi ya pauni milioni 300 katika matumizi ya dirisha hili la usajili, ikiwa ni sehemu ya mpango mkubwa wa De Zerbi wa kujenga upya kikosi baada ya Spurs kumaliza msimu uliopita katika nafasi ya 17. “Tunataka kurejesha Tottenham kwenye ushindani wa juu,” ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo huku ikiendelea kutafuta wachezaji wengine, akiwemo mshambuliaji wa Manchester City, Omar Marmoush.

Tottenham Yakamilisha Usajili wa Savinho Kutoka Manchester United kwa £75MKwa upande wa Manchester City, mauzo ya Sávio yanaweza kuwa rekodi mpya ya mauzo ya klabu hiyo iwapo thamani ya dili itafikia pauni milioni 85, na kuvuka pauni milioni 82 zilizolipwa na Atlético Madrid kumsajili Julian Alvarez mwaka 2024. Tottenham sasa inatumaini usajili wa Sávio utasaidia kuboresha kiwango cha timu na kuanza safari ya kurejea katika ushindani wa juu.

Acha ujumbe

Meridianbet

Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.