Klabu ya Tottenham Hotspur imekamilisha usajili wa kiungo Mateus Fernandes kutoka West Ham United kwa ada ya pauni milioni 85, usajili ambao umeweka rekodi mpya ya klabu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa akiwaniwa pia na Manchester United, lakini ameichagua Tottenham na kusaini mkataba wa muda mrefu wa kuitumikia timu hiyo ya London Kaskazini.
Fernandes amesema ana furaha kubwa kujiunga na Spurs, akieleza kuwa mazungumzo yake na kocha Roberto De Zerbi yalikuwa na ushawishi mkubwa katika uamuzi wake. “Nina furaha sana kuchukua hatua hii mpya. Tottenham ni klabu kubwa na kocha alikuwa sababu muhimu iliyonifanya nichague kujiunga hapa. Tunafikiria soka kwa mtazamo mmoja wa kupambana na kushinda kila mchezo. Siwezi kusubiri kukutana na mashabiki na kutoa kila kitu kwa ajili ya klabu,” alisema Fernandes.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Usajili huo umevunja rekodi ya awali ya Tottenham ya pauni milioni 65 waliyoitumia kumsajili Dominic Solanke kutoka Bournemouth. Katika dirisha hili la usajili, Spurs pia wamewasajili Jan Paul van Hecke kwa pauni milioni 52 kutoka Brighton, huku Andy Robertson, Marcos Senesi na Martin Dubravka wakijiunga kwa uhamisho wa bure. Aidha, klabu hiyo inaendelea na mazungumzo ya kumsajili kiungo Sandro Tonali kutoka Newcastle United.
Kocha Roberto De Zerbi amesema amekuwa akimfuatilia Fernandes kwa muda mrefu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza na mpira pamoja na bidii yake uwanjani. “Mateus ana ubora mkubwa akiwa na mpira, ana akili ya mchezo na anafanya kazi kwa nguvu kwa ajili ya timu. Ana uwezo wa kuhimili presha na kuamua matokeo katika nyakati ngumu. Ninaamini Tottenham ni sehemu sahihi kwake kuendelea kukua na nina hamu ya kuanza kufanya kazi naye,” alisema De Zerbi.
Fernandes alijiunga na West Ham msimu uliopita akitokea Southampton kwa ada ya takribani pauni milioni 40 baada ya Southampton kushuka daraja. Alicheza mechi zote 38 za Ligi Kuu England, akifunga mabao manne, ingawa West Ham ilimaliza msimu kwa kushuka daraja. Kiungo huyo pia alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya taifa ya Ureno mwezi Aprili, lakini hakujumuishwa kwenye kikosi cha kocha Roberto Martinez kwa ajili ya michuano ya Dunia la majira haya ya joto.


