TPLB Yahamisha Mchezo wa Prison, Yanga Kupigwa Dodoma

Bodi ya ligi (TPLB) imetangaza rasmi mabadiliko ya uwanja kwa mchezo namba 30 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Tanzania Prisons na Yanga sc uliopangwa kuchezwa Machi 12, 2026. Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika katika uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 alasiri.

TPLB Yahamisha Mchezo wa Prison, Yanga Kupigwa Dodoma

Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, mchezo huo sasa utafanyika siku hiyohiyo lakini katika uwanja wa  Jamhuri Dodoma kuanzia saa 2:00 usiku. Mabadiliko hayo yamefanywa kufuatia kufungwa kwa Uwanja wa Sokoine baada ya maelekezo kutoka Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Awali klabu ya Tanzania Prisons ilitoa taarifa kwa umma ikieleza kuwa kufungwa kwa uwanja wa Sokoine kungeifanya timu hiyo kucheza michezo yake ya nyumbani katika uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi Tabora kwa muda, wakati ukarabati ukiendelea.

TPLB Yahamisha Mchezo wa Prison, Yanga Kupigwa Dodoma

Hata hivyo, baada ya tathmini na maamuzi ya bodi ya ligi, imeamuliwa kuwa mchezo huo muhimu dhidi ya Yanga sc uhamishiwe katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma badala ya Tabora kama ilivyotangazwa awali na klabu ya Tanzania Prisons. Sababu ya mabadiliko hayo ni kufungwa rasmi kwa Uwanja wa Sokoine na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF, hatua iliyolazimisha wadau wa ligi kufanya marekebisho ya haraka ili kuhakikisha ratiba ya ligi inaendelea bila kuathiri ushindani wa mashindano hayo.

TPLB Yahamisha Mchezo wa Prison, Yanga Kupigwa Dodoma

Bodi ya ligi TPLB imewataka wadau wote wa mchezo huo wakiwemo klabu shiriki, mashabiki na waandaaji wa maandalizi kuzingatia mabadiliko hayo mapya ya uwanja na muda wa mchezo ili kuhakikisha maandalizi yanaenda sawa kwa pambano hilo la Ligi Kuu Bara.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.