Tuchel Afichua Athari za Mapumziko ya Maji Yanaharibu Ladha ya Soka

Kocha wa England, Thomas Tuchel, amesema Mapumziko ya Maji Yanaharibu Ladha ya Soka, amesema mapumziko ya kunywa maji yaliyoanzishwa kwenye mashindano ya Dunia 2026 yanaathiri mwenendo wa mechi kuliko ilivyodhaniwa awali, huku akidai kuwa yanaharibu kasi na utambulisho wa mchezo wa soka.

Tuchel Afichua Athari za Mapumziko ya Maji Yanaharibu Ladha ya SokaFIFA ilianzisha mapumziko hayo ya dakika tatu katikati ya kila kipindi kutokana na joto kali katika miji inayoshiriki kuandaa mashindano hayo nchini Marekani, Canada na Mexico. Hata hivyo, uamuzi huo umeendelea kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka, baadhi wakidai kuwa unavuruga mtiririko wa mchezo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza kuelekea mchezo wa England dhidi ya Ghana katika Kundi L, Tuchel alisema mapumziko hayo yanafanya mechi kugawanyika kana kwamba inachezwa katika robo nne tofauti. “Nadhani mapumziko ya maji yanakatiza mchezo na kubadilisha utambulisho wa mechi ya soka zaidi ya tulivyotarajia. Zamani tulikuwa na mapumziko kama haya wakati wa joto kali sana, lakini yalikuwa mafupi na katika mechi chache tu,” alisema kocha huyo.

Tuchel Afichua Athari za Mapumziko ya Maji Yanaharibu Ladha ya SokaLicha ya baadhi ya mechi kutochezwa katika hali ya joto kali, Shirikisho limeamua mapumziko hayo yawepo katika kila mchezo kwa ajili ya usawa na ulinganifu wa mashindano. Hata hivyo, Tuchel anaamini kuwa hali hiyo inafanya kuwa vigumu kwa timu kujenga na kudumisha kasi ya mchezo kwa muda mrefu.

Tuchel Afichua Athari za Mapumziko ya Maji Yanaharibu Ladha ya Soka“Kama kocha, bila shaka napenda kuwa na nafasi ya kuzungumza na wachezaji wangu, lakini kwa ujumla napenda zaidi soka linapochezwa bila kusimamishwa mara kwa mara. Ni vigumu kujenga momentum na kuendelea nayo. Hilo ni sehemu ya uzuri wa mchezo, na mapumziko haya yanaondoa jambo hilo,” aliongeza Tuchel.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.