Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel ameeleza kuwa anaamini sana kuwa atafanikiwa kushinda taji la UEFA msimu huu atakapocheza na Manchester City baadae mwezi huu.

Chelsea na Manchester City watakutana tena katika fainali ya Champions league tarehe 29 mwezi huu. Bado haijajulikana ni uwanja gani utatumika kutokana na ule wa awali kule Instabul kutiliwa shaka baada ya Uturuki kuwekewa vikwazo na Uingereza.

Katika mahojiano maalum, Tuchel alisema kuwa ushindi waliopata dhidi ya Manchester City juzi umewatengenezea hari na imani kubwa ya kuchukua ubingwa wa UEFA toka wafanye hivyo mwaka 2012 dhidi ya Bayern Munich.

Ndiyo, mchezo huu umetupa imani kubwa ya kushinda fainali dhidi ya City, na tunaamini tunaweza kufanya hivyo kama tulivyofanya nyuma. Tutajaribu kutunza hali tuliyonayo ya kujiamini tutakapofika Istanbul, kwani tutakuwa na lengo moja tu la kushinda taji hiloalisema Tuchel

Tuchel pia aliongeza kuwa michezo wanayocheza hivi sasa itawaanda zaidi kuelekea kwenye fainali hiyo kubwa ambayo mashabiki wa the Blues walikosa kwa muda mrefu.

PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Tuchel, Tuchel: Chelsea Wana Imani Kubwa Ya Kushinda UCL!, Meridianbet

CHEZA HAPA

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa