Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amefichua kuwa historia ya hivi karibuni majeraha ya N’Golo Kante bila shaka itazingatiwa katika mazungumzo ya kandarasi na kiungo huyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa Stamford Bridge, na The Blues wanataka kumbakiza klabuni hapo.

Hata hivyo, Kante alicheza mechi 26 pekee za ligi kuu msimu uliopita idadi yake ya pili kwa udogo tangu aende Uingereza mwaka 2015 na kwa sasa hayuko vizuri kutokana na tatizo la misuli.

 

Thomas Tuchel: N'golo Kante Tutazingatia Kila Kitu Kwenye Mkataba Wake.

Tuchel amekiri kwamba msururu huu wa majeruhi wa hivi karibuni utaathiri aina ya ofa ya kandarasi ambayo Kante atapokea kutoka kwa Chelsea.

 

Thomas Tuchel: N'golo Kante Tutazingatia Kila Kitu Kwenye Mkataba Wake.

Alipoulizwa iwapo rekodi ya majeraha ya Kante inaweza kupuuzwa katika mazungumzo, Tuchel alijibu:

“Huwezi. Unapaswa kuzingatia kila kitu kilichopo mezani na mezani ni uwezo wake, ushawishi wake, na ubora wake, Lakini pia kwenye meza, bila shaka, ni umri wake, mshahara wake na kiwango chake cha majeruhi. Kutoka hapo unajenga picha nzima na kujaribu kutafuta suluhisho.”


Tandika jamvi lako la leo na Meridianbet HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa