“Tulimpa Nafasi Messi” Petković Akiri Makosa Baada ya Kipigo Argentina

Kocha wa Algeria Vladimir Petković amesema makosa ya kikosi chake yaliwasaidia nyota wa Argentina Lionel Messi kufunga hat-trick na kuisambaratisha Algeria kwa mabao 3-0 katika mchezo wa michuano ya Dunia uliochezwa Kansas City.

“Tulimpa Nafasi Messi” Petković Akiri Makosa Baada ya Kipigo ArgentinaPetković amesema timu yake ilimpa Messi nafasi kubwa ya kucheza na hivyo kurahisisha kazi yake, akisisitiza kuwa ubora wa mchezaji huyo hauwezi kupuuzwa. Amesema: “Ubora wake haubadiliki kwa sababu tunazungumzia mchezaji ambaye ameshinda Ballon d’Or mara nyingi sana katika maisha yake ya soka.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo ameongeza kuwa Algeria ilifanya makosa ya kiufundi yaliyosababisha mabao mawili ya awali, jambo lililompa Messi nafasi ya kuongoza mchezo kwa urahisi zaidi. Amesema: “Kwa bahati mbaya tulimpa nafasi katika bao la kwanza na la pili, na tukamrahisishia kufunga.”

“Tulimpa Nafasi Messi” Petković Akiri Makosa Baada ya Kipigo ArgentinaPetković pia ameeleza kuwa Argentina ina mfumo unaomzunguka Messi na kumsaidia kufanya vizuri zaidi uwanjani, akisisitiza kuwa Argentina ilitengeneza mashambulizi mengi kupitia kwake katika mchezo huo. Amesema: Argentina ina wachezaji wanaomsaidia na kwa miaka mingi ameendelea kufanya mambo makubwa sana.”

“Tulimpa Nafasi Messi” Petković Akiri Makosa Baada ya Kipigo ArgentinaHata hivyo, amewataka wachezaji wake kujifunza kutokana na makosa hayo na kujiandaa kwa michezo iliyobaki ya Kundi J dhidi ya Jordan na Austria, akisema wanahitaji kurekebisha makosa yao na kuongeza imani ili kupata matokeo bora katika mechi zijazo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.