Miamba ya Ujerumani Bayern wanampango wa kubeba Bundesliga mara ya tisa mfululizo kwa msimu 2020-21 na usiku wa leo watawakaribisha Schalke katika dimba la Allianz Arena.

Mabingwa hao wa Ulaya wataendeleza utawala wao na wanaonekana kuwa imara na kutohofia wapinzani.

Ingawa watamkosa mchezaji Thiago Alcantara ambaye yupo njiani kuelekea Liverpool, Bayern tayari wana kikosi cha kuvutia na sasa kimezidi kuimarika baada ya kumuongeza Leroy Sane kutoka Manchester City.

Mabingwa hao wa Bundesliga walishinda michezo 21 katika mashindano na hawajapoteza tena tangu wapoteze kwa Borussia Monchengladbach mwezi Disemba mwaka uliyopita.

Bayern Munich chini ya kocha Hans-Dieter Flick.

Timu hiyo iliyo chini ya mwalimu Hans-Dieter Flick walishinda ubingwa wa Bundesliga kwa mara nyingine huku Robert Lewandowski akiwa ndiyo kinara wa upachikaji mabao katika ligi hiyo.

Mpoland huyo mwenye umri wa miaka 32 alitikisa nyavu za wapinzani mara 34 katika michezo 31 ya Bundesliga na kupata hat-trick katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Schalke mwezi Agosti 2019.

Uchambuzi: Bayern Munich vs Schalke.
Wachezaji wa Bayern Munich wakisherehekea goli dhidi ya Schalke 04

Schalke waligongelewa nyundo 5-0 katika dimba la Allianz Arena mwezi Januari na Bayern iliwaondoa katika michuano ya DFB Cup mwezi Machi.

Schalke walimaliza nafasi ya 12 katika Bundesliga baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo 16 walipoteza michezo 10 na kufunga mara saba pekee.

Licha ya Bayern kumkosa Kingsley Coman ambaye kajichimbia nyumbani kutokana kuwa na COVID-19, Schalke watakabiliana na vita ngumu pale Allianz.

Idadi ndogo ya mashabiki wataruhusiwa kushuhudia mechi za Bundesliga,msimu huu lakini jioni ya Leo gemu itapigwa bila mashabiki.

Meridianbet tumekuwekea odds za ushindi katika mechi hii GUSA HAPA kufanya ubashiri wako.


SHINDA NA MERIDIANBET!

Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.

Cheza Sasa.

35 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa