Uchambuzi:Mchezo wa Kirafiki England vs Wales.

Bosi wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate atatoa nafasi kwa wachezaji makinda waweze kuonesha walicho nacho pale Wales itakapo tembelea viunga vya Wembley jioni ya leo (Saa nne kamili usiku saa za afrika mashariki).

The Three Lions, watajipima ubavu na majirani zao Wales kuulekea katika michuano ya Nations League kwa ratiba itakayo ikutanisha Uingereza na Belgium na Denmark.

Straika wa Everton Dominic Calvert-Lewin anajiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza katika timu ya wakubwa baada ya kuwa na moto katika msimu mpya wakati mchezaji mwenzake ambaye pia ni mgeni Buyako Saka na Harvey Barnes naye pia anatarajiwa kuchezeshwa.

Jack Grealish na Conor Coady wote ndani ya kikosi hii ni baada ya kufanya vizuri katika mchezo wa kwanza walipocheza dhidi ya Danes mwezi uliyopita, magolikipa Nick Pope na Dean Henderson watakuwa kando kumsaidia golikipa namba moja Jordan Pickford.

Uchambuzi:Mchezo wa Kirafiki England vs Wales.
Ryan Giggs na Gareth Southgate

Timu ya Ryan Giggs,Wales ambao ni wageni wa Uingereza hajapoteza katika michezo nane iliyopita watafanya mabadiliko kutokana kukosekana kwa idadi kubwa ya wachezaji.

Gareth Bale bado hajawa fit kucheza, wakati Joe Allen,Hal Robson-Kanu na Tom Lockyer wote wanauguza majeraha.

The Dragon itamkosa pia kiungo wao Aaron Ramsey, ambaye anatumikia muda wa kujitenga akiwa Juventus baada ya watumishi wawili wa klabu hiyo ya Turin kukutwa na maambukizi ya COVID-19.

Southgate atalazimika kuwakumbusha tena vijana wake majukumu yao wakati wakiwa wanawakilisha taifa lao la Uingereza.

Tammy Abraham,Ben Chilwell na Jadon Sancho wataukosa mchezo huu baada ya kuvunja sheria za Kujikinga na COVID-19 kwa kufika sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi zaidi ya sita wiki iliyopita lakini pia Greenwood na Phil Foden wameachwa katika kikosi cha Southgate.

Uchambuzi:Mchezo wa Kirafiki England vs Wales.
Tammy Abraham, Jadon Sancho na Ben Chilwell

Ingawa matokeo ya leo hayana umuhimu sana lakini Southgate anatarajia matokeo chanya kutoka katika timu yake baada ya kuwa na kiwango kibovu mechi dhidi ya Iceland na Denmark.

Je Wajua?

England haijapoteza katika michezo nane ya kirafiki tangu ilifungwa 3-2 na Ufaransa mwaka 2017.The Three Lions imeruhusu magoli mawili pekee katika michezo yote nane.

Raheem Sterling amefunga magoli 11 katika mechi 13 za England lakini ameshindwa kuvamia nyavu katika michezo 17 ya kirafiki.

Wales wameshinda mara moja pekee katika mechi 17 walizokutana na England katika dimba la Wembley ushindi wao huo mmoja waliupata mwaka 1977 goli pekee lililofungwa na Leighton James kwa mkwaju wa penati.


Weka Pesa kwa Airtel Money!

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!

Soma Zaidi

34 Komentara

    itakuwa bonge la mechi

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    game kali sana

    Jibu

    Hii Ni bonge la mechi

    Jibu

    Bonge la game hilo

    Jibu

    Game kali

    Jibu

    Plan yake nzur san

    Jibu

    Bonge la game

    Jibu

    Mtanange matata sana

    Jibu

    Bonge la makala

    Jibu

    England ya Southgate imekuwa na kikosi kipana na wachezaji mahiri wanaotakiwa kufanya kiti kwa mashabiki wenye wazimu wa mpira wa England wenye hamu kuona taifa lao linarudia historia ya mwaka 1966 ilipochukua Ubingwa wa dunia#meridianbettz

    Jibu

    Itakuwa mechi ya kibabe

    Jibu

    Itakua hatarii

    Jibu

    Shuhuli itakua nzito maana wales hatokubali kizembe apigwe hapo ndio itakua kazi ipo

    Jibu

    Mtanange mkal sana 👍

    Jibu

    kazi itakuwepo

    Jibu

    Wote wababe

    Jibu

    Mtanange utakuwa sio wa kitoto mechi zote kali

    Jibu

    Itakua bonge la mechi

    Jibu

    Duuuh hptoshi

    Jibu

    Mechi ngumu

    Jibu

    His machi itakuwa kali

    Jibu

    🔥

    Jibu

    Bonge la game

    Jibu

    England huenda wakafanya makubwa safari hii

    Jibu

    England win

    Jibu

    Wales win

    Jibu

    Mechi kalii

    Jibu

    England msimu huu wapo motooo

    Jibu

    England ni shida ingine tena

    Jibu

    Don’t miss

    Jibu

    Hii si ya kuikosa kabsa

    Jibu

    England ya Southgate imekuwa na kikosi kipana na wachezaji mahiri wanaotakiwa kufanya kiti kwa mashabiki wenye wazimu wa mpira wa England wenye hamu kuona taifa lao linarudia historia ya mwaka 1966 ilipochukua Ubingwa wa dunia

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.