Niki iangalia Brazil nagundua mpira wa Miguu una mambo mengi sana ambayo mengi yamefichika, ni mazito, ni mazito ni mazito sana! Mpira wa miguu hauchezwi tu uwanjani bali unaanzia nje kabisa
Ufaransa aliwahi kulalama kuhusu drones kurushwa hewani kambini kwake kwenye fainali za kombe la dunia 2014 Brazil, waligundua kuna wapinzani wanawachunguza, ni sehemu tu ya Umafia kwenye mpira
Mataifa makubwa wanachezeana rafu nyingi sana kijasusi, watu wanaajiri watu kwa ajili ya kazi za upepelezi haswa kwenye mifumo ya nchi kwenye soka, mbinu zao na Falsafa zao, watu wanalipwa kwa kazi hiyo
Kwa miaka mingi sana timu ya Taifa ya Ujerumani ilikuwa ikichunguzwa, watu walitaka kujua kazi ya Project ya miaka 10 baada ya World Cup 2002, chini ya Mtaalam mmoja anaitwa Wolfgang! Kwenye blueprint ile mambo mengi yalifichika
Mataifa mengi yalitaka kutumia teknolojia na Ujasusi kubaini ubora wa Ujerumani, haikuwa rahisi kutumia teknolojia pekee maana Wajerumani ndio Taifa linaloaminiwa zaidi na FIFA kwenye masuala ya teknolojia, hata Goal Line inaendeshwa na Wajerumani
Brazil alikufaje 7-1??
Sasa kuelekea kombe la dunia 2014, Maafisa wa soka wa Brazil waliketi pale Granja Comary, Rio De Janeiro, kwenye kikao chao walimteua Eduardo Cesar Daud Gaspar, watu wengi mnamtambua kama EDU, ndio ni huyo Mkurugenzi wa Ufundi wa Arsenal
Edu kipindi hicho ni Mkurugenzi wa Corinthians akichukua nafasi ya William Machado 2011, ni Edu huyu alitumwa kuelekea Ujerumani na Hispania kwa ajili ya kuzisoma timu zao, Mataifa haya yalitambulika kama hatari zaidi
Edu alitumwa kama Jasusi, na alianza kuwasili Nchini Ujerumani, mchoro wake ukiwa ni Berlin, Munich na Ruhr region (Ukanda wa Viwanda) alienda kwa ajili ya Ujasusi
Bahati mbaya kwenye Ujasusi kuna vitu viwili INTELLIGENCE na COUNTER INTELLIGENCE
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.