United Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mnunuzi wa Andre Onana

Kipa wa Manchester United, Andre Onana, anatarajiwa kutorejea kikosini msimu ujao licha ya taarifa kuwa yuko tayari kupigania nafasi yake Old Trafford.

United Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mnunuzi wa Andre OnanaRipoti zinaeleza kuwa kipa huyo wa kimataifa wa Cameroon ana nia ya kurejea katika maandalizi ya msimu mpya ili kujithibitisha kwa kocha mpya, akiamini bado ana nafasi ya kuchangia ndani ya klabu hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Onana, ambaye msimu huu amekuwa kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor, anaamini bado ana kazi ambayo hajamaliza Manchester United na hataki kuondoka bila kupewa nafasi ya kweli ya kurejea katika kiwango chake.

United Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mnunuzi wa Andre OnanaHata hivyo, vyanzo vya ndani vinaeleza kuwa msimamo wa United uko wazi, wakisisitiza kuwa: “Klabu inaendelea kutafuta timu nyingine kwa ajili ya Onana katika dirisha la majira ya joto ikiwa itahitajika.”

 

Katika hatua nyingine, mabadiliko yanatarajiwa pia katika eneo la makipa, ambapo kipa namba mbili Altay Bayındır anaweza kuondoka, huku kurejea Uturuki kukionekana kama uwezekano mkubwa. Aidha, klabu hiyo inapanga kusajili kipa mpya wa akiba kama sehemu ya maboresho ya kikosi.

United Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mnunuzi wa Andre OnanaSababu za kifedha pia zinatajwa kuwa muhimu, huku mshahara wa Onana unaokadiriwa kuwa pauni 175,000 kwa wiki ukionekana kuwa mkubwa kwa nafasi ya kipa wa akiba. Wakati huohuo, kipa Senne Lammens ameonyesha kiwango kizuri tangu kuwa chaguo la kwanza, jambo linaloifanya United kuridhika na mipango yao ya usajili. “Isipokuwa kutokee mabadiliko makubwa, itashangaza kumuona Onana akirejeshwa kikosini msimu ujao,” kilieleza chanzo cha karibu na klabu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.