“Ureno Tunaweza Kushinda Taji la Dunia” Fernandes Aweka Msisitizo wa Ubingwa

Kiungo wa ushambuliaji Bruno Fernandes amesema timu ya taifa ya Ureno imejipanga kupigania ubingwa wa Dunia 2026, lakini amesisitiza safari hiyo haitakuwa rahisi wanapojiandaa na mchezo wao wa kwanza wa Kundi K dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Fernandes amesema hatua ya kwanza muhimu ni kuhakikisha wanatoka kwenye kundi lao lenye ushindani mkubwa dhidi ya Colombia na Uzbekistan.

“Ureno Tunaweza Kushinda Taji la Dunia” Fernandes Aweka Msisitizo wa UbingwaFernandes amesema: Timu bora ni ile inayoshinda, kwa hiyo tunatumaini mwisho wa mashindano haya tutakuwa tukiitwa hivyo. Tuna kikosi kizuri, vipaji vikubwa na tumeungana kama timu.” Ameongeza kuwa Ureno inalenga kuchukua kila mchezo kwa wakati wake bila kuwaza mbali zaidi ya mechi inayofuata dhidi ya Congo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumzia wapinzani wao, Fernandes amewatahadharisha wachezaji wenzake kutoidharau Democratic Republic of the Congo akisema ni timu yenye nguvu na kasi kubwa hasa kwenye mashambulizi ya kushtukiza. Amesema: “Tunaijua Congo ni timu yenye uwezo mkubwa, wachezaji wenye nguvu na wanaoweza kutuumiza kwenye mashambulizi ya kushtukiza na mipira ya juu.”

“Ureno Tunaweza Kushinda Taji la Dunia” Fernandes Aweka Msisitizo wa UbingwaFernandes pia ameeleza furaha yake kucheza pamoja na nahodha wa Cristiano Ronaldo katika mashindano hayo ya dunia, akisema ni heshima kubwa kwa kila mchezaji wa Ureno. Ameongeza kuwa Ronaldo anaendelea kuwa na hamasa kubwa kila anapovaa jezi ya taifa na ni mfano kwa kizazi kipya cha wachezaji.

“Ureno Tunaweza Kushinda Taji la Dunia” Fernandes Aweka Msisitizo wa UbingwaKatika sehemu ya majonzi, Fernandes amemkumbuka aliyekuwa mchezaji mwenza Diogo Jota, akisema bado ni sehemu ya kikosi chao kiroho. Amesema Jota alikuwa mchezaji mwenye nidhamu, mcheshi na mwenye mapenzi makubwa na taifa lake, na wataendelea kumkumbuka katika safari yao ya mashindano ya Dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.