Nahodha wa Liverpool Virgil Van Dijk ameongezewa adhabu ya mchezo mmoja na faini ya paundi laki moja baada ya kukiri kutoa maneno makali kwa mwamuzi baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle.
Beki Van Dijk alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Newcastle baada ya kufanya madhambi, Lakini wakati anatoka alionekana akitoa maneno kwa mwamuzi jambo ambalo limemfanya kufungiwa na kupigwa faini.Adhabu ya beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi ilikua imalizike katika mchezo ambao aliukosa na klabu yake ya Liverpool kushinda kwa mabao matatu dhidi ya Aston Villa hivo beki huyo ataukosa mchezo dhidi ya Wolves utakaopigwa Septemba 16.
Mchezaji huyo baada ya mahujiano alikiri kua alitoa maneno ya matusi kwa msimamzi wa mcheza na shirikisho la soka nchini Uingereza kuamua kumpa adhabu beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi baada ya kukiuka kanuni za ligi hiyo.Kukosekana kwa beki Van Dijk katika mchezo mwingine inaendelea kua pigo kwa klabu ya Liverpool, Kwani beki huyo amekua muhimili mkubwa klabuni hapo tangu atue kwenye timu hiyo mwezi Januari mwaka 2018 akitokea Southampton.