Vigogo wa Jiji la Manchester Wapigana Kuinasa Saini ya Cucurella

Manchester United na Manchester City zimeingia kwenye ushindani mkali wa kuwania saini ya beki wa kushoto wa Chelsea, Marc Cucurella, baada ya nyota huyo kuonyesha nia ya kuondoka Stamford Bridge katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi.

Vigogo wa Jiji la Manchester Wapigana Kuinasa Saini ya CucurellaRipoti zinaeleza kuwa Cucurella mwenye umri wa miaka 27 tayari amewaarifu viongozi wa Chelsea kuhusu dhamira yake ya kutafuta changamoto mpya, huku klabu hiyo ya London ikiwa tayari kumsikilizia ofa itakayokuwa kati ya Euro milioni 40 hadi 50.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Manchester United wanamwona Cucurella kama moja ya suluhisho muhimu kwa tatizo lao la muda mrefu katika nafasi ya beki wa kushoto,” kilieleza chanzo cha karibu na mazungumzo hayo, huku kocha wa United akitajwa kuhitaji mchezaji mwenye uzoefu wa Ligi Kuu England.

Vigogo wa Jiji la Manchester Wapigana Kuinasa Saini ya CucurellaKwa upande wa Manchester City, ingawa wana wachezaji kadhaa wanaoweza kucheza nafasi hiyo, viongozi wa klabu hiyo bado wanaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya sakata hilo. “City hawajaondoa uwezekano wa kufanya mazungumzo iwapo mazingira yatakuwa mazuri kwao,” kiliongeza chanzo hicho.

Vigogo wa Jiji la Manchester Wapigana Kuinasa Saini ya CucurellaHata hivyo, si vigogo wa Manchester pekee wanaomuwinda beki huyo wa Hispania. Klabu za Atlético Madrid na Barcelona pia zimeonyesha nia ya kupata huduma zake, huku taarifa zikidai kuwa Cucurella mwenyewe angependa kurejea La Liga ikiwa ataondoka Chelsea katika kipindi hiki cha usajili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.