Vijana wa Real Madrid Juvenil A WaPongezwa Baada ya Ubingwa wa UEFA Youth League

Kabla ya mchezo wa LaLiga kati ya Real Madrid na Deportivo Alavés, kikosi cha vijana cha Juvenil A cha Real Madrid kiliingia uwanjani katika hafla maalum ya kupongezwa baada ya kutwaa ubingwa wa vijana wa Ulaya, UEFA Youth League.

Vijana wa Real Madrid Juvenil A WaPongezwa Baada ya Ubingwa wa UEFA Youth LeagueTukio hilo lilifanyika katika uwanja wa Santiago Bernabéu mbele ya mashabiki wengi waliokuwa wamejitokeza kushuhudia mchezo huo. Vijana hao waliandamana uwanjani wakiwa na medali zao za ushindi, wakipita katikati ya wachezaji wa timu kubwa huku wakisindikizwa na makofi makubwa kutoka kwa mashabiki. Wachezaji wa timu ya wakubwa pia walijiunga katika kutoa pongezi hizo kama ishara ya kuthamini mafanikio ya akademia ya klabu hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika tukio hilo, baadhi ya nyuso za wachezaji wa wakubwa zilionekana kuwa na mchanganyiko wa hisia, ambapo pamoja na kupiga makofi, ilionekana pia kama kuna ujumbe wa kuwakumbusha umuhimu wa kujitathmini kutokana na mafanikio ya vijana hao. Hali hiyo ilizua hisia tofauti miongoni mwa watazamaji uwanjani.

Vijana wa Real Madrid Juvenil A WaPongezwa Baada ya Ubingwa wa UEFA Youth LeagueKwa upande mwingine, tukio hilo limeonekana kama sehemu ya utamaduni wa klabu ya Real Madrid kuhamasisha ushindani na kuonyesha njia ya mafanikio kutoka akademia hadi timu ya wakubwa. Wengi wanaamini kuwa ni ujumbe wa kimotisha zaidi kuliko kejeli, ukilenga kuonyesha kiwango cha juu cha vijana wa klabu hiyo.

Vijana wa Real Madrid Juvenil A WaPongezwa Baada ya Ubingwa wa UEFA Youth LeagueBaada ya sherehe hiyo, macho yote yalielekezwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Alavés, ambapo Real Madrid waliingia uwanjani wakiwa na shinikizo la kuendeleza matokeo chanya. Hata hivyo, tukio la vijana Juvenil A lilibaki kuwa moja ya matukio yaliyozua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.