Vilabu vya EPL Vamnyemelea Bowen Endapo West Ham Watashuka Daraja

Nahodha wa West Ham United, Jarrod Bowen, anaweza kulazimika kufanya uamuzi mkubwa kuhusu mustakabali wake wa soka msimu huu wa kiangazi ikiwa timu hiyo itashuka daraja kutoka Ligi Kuu England.

Vilabu vya EPL Vamnyemelea Bowen Endapo West Ham Watashuka DarajaWest Ham wanaingia kwenye mchezo wao wa mwisho wa msimu dhidi ya Leeds United wakiwa kwenye vita ya kusalia EPL, huku vilabu kadhaa vikubwa vikionesha nia ya kumhitaji Bowen. Inaelezwa kuwa Bowen bado ana nia ya kuendelea kubaki West Ham iwapo timu hiyo itaepuka kushuka daraja Jumapili hii. Hata hivyo, kushuka kwenda Championship kunaweza kubadilisha kabisa hali hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, wachezaji wa West Ham wana kipengele cha kupunguziwa mshahara kwa asilimia 50 iwapo timu itashuka daraja, jambo ambalo linaweza kuifanya klabu ishindwe kuzuia ofa kubwa kwa nyota wake huyo.

Vilabu vya EPL Vamnyemelea Bowen Endapo West Ham Watashuka DarajaBowen, ambaye alikosa nafasi kwenye kikosi cha Thomas Tuchel cha England kuelekea Kombe la Dunia, ameendelea kuvutia vilabu vingi kutokana na uwezo wake wa uongozi na mchango mkubwa wa mabao na mashambulizi.

Vilabu vya EPL Vamnyemelea Bowen Endapo West Ham Watashuka Daraja“West Ham hawatamuuza Bowen kwa bei rahisi hata kama watashuka daraja. Thamani yake bado ipo juu kutokana na kiwango chake bora cha muda mrefu katika Premier League.

Vilabu vya EPL Vamnyemelea Bowen Endapo West Ham Watashuka DarajaMshambuliaji huyo mwenye miaka 29 ana mkataba hadi mwaka 2030, lakini anatarajiwa kuvutia ofa nyingi kutoka vilabu vya EPL iwapo West Ham watashindwa kubaki ligi kuu. Inaelezwa kuwa Bowen angependa kubaki jijini London iwapo ataondoka West Ham, huku Tottenham Hotspur ambao wanaweza kubaki EPL kwa gharama ya West Ham mwishoni mwa wiki hii  wakitajwa kuwa miongoni mwa vilabu vinavyofuatilia hali yake. Vilabu vingine vinavyomuwania ni Chelsea, Liverpool na Newcastle United.

Vilabu vya EPL Vamnyemelea Bowen Endapo West Ham Watashuka DarajaWest Ham watalazimika kuifunga Leeds United katika Uwanja wa London Stadium na wakati huo huo kutegemea Everton kuifunga Tottenham ili kuhakikisha wanabaki kwenye Ligi Kuu England msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.