Vozinha Afunguka Sababu ya Kulia Baada ya Sare ya 0-0 Dhidi ya Hispania

Golikipa mkongwe wa Cape Verde, Josimar Dias maarufu kama Vozinha, amefichua sababu iliyomfanya ashindwe kuzuia hisia zake na kulia baada ya mechi ya michuano ya Dunia 2026 dhidi ya Hispania kumalizika kwa sare tasa ya 0-0.

Vozinha Afunguka Sababu ya Kulia Baada ya Sare ya 0-0 Dhidi ya HispaniaVozinha mwenye umri wa miaka 40 alikuwa shujaa wa Cape Verde katika mchezo huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu na kusaidia timu yake kupata alama muhimu dhidi ya moja ya mataifa makubwa ya soka duniani. Baada ya filimbi ya mwisho, kamera zilimnasa akilia jambo lililozua maswali mengi miongoni mwa mashabiki.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo huo, kipa huyo alieleza kuwa machozi yake yalitokana na kumbukumbu za watu waliomlea ambao hawakuweza kushuhudia mafanikio hayo. “Nililia baada ya mechi kwa sababu nilikulia na babu na bibi zangu nilipokuwa mtoto, na hawakuweza kuwepo hapo. Walifariki miaka michache iliyopita,” alisema Vozinha.

Vozinha Afunguka Sababu ya Kulia Baada ya Sare ya 0-0 Dhidi ya HispaniaKipa huyo pia alifichua kuwa mama yake alikosa nafasi ya kushuhudia moja kwa moja mechi hiyo kutokana na changamoto za usafiri. “Mama yangu pia hakuweza kuwa hapa kutokana na tatizo la kupata viza na gharama zilizohusika. Hatukufanikiwa kukamilisha mchakato huo kwa wakati,” aliongeza.

Vozinha Afunguka Sababu ya Kulia Baada ya Sare ya 0-0 Dhidi ya HispaniaMbali na kung’ara uwanjani, Vozinha ameshuhudia ongezeko kubwa la umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya mchezo huo. Idadi ya wafuasi wake kwenye Instagram imeongezeka kwa kasi kutoka takribani elfu 50 hadi kufikia zaidi ya milioni 6, huku mashabiki kutoka sehemu mbalimbali duniani wakimpongeza kwa kiwango chake bora na simulizi yake ya kugusa hisia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.