Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeibua mjadala mkubwa baada ya kutangaza waamuzi watano wote kutoka Argentina watakaosimamia mchezo wa robo fainali ya michuano ya Dunia kati ya Ufaransa na Morocco utakaochezwa kesho july 9.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na FIFA, Facundo Tello atakuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Juan Pablo Belatti na Gabriel Chade kama waamuzi wasaidizi, huku Dario Herrera akiwa mwamuzi wa nne na Christian Navarro akiteuliwa kuwa mwamuzi wa akiba. Waamuzi hao wote ni raia wa Argentina.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hatua hiyo imewashangaza wadau wengi wa soka kwani ni mara ya kwanza katika michuano hiyo waamuzi wote wa mchezo mmoja kutoka taifa moja kuteuliwa kusimamia mechi ya michuano ya Dunia. Baadhi ya mashabiki wameonyesha wasiwasi kuhusu uamuzi huo, ingawa FIFA haijatoa maelezo ya ziada kuhusu uteuzi huo.
Wakati mjadala ukiendelea, baadhi ya watu wameendelea kutoa madai kwamba Argentina imekuwa ikipata upendeleo kutoka FIFA ili iweze kutetea taji lake la Dunia. Hata hivyo, madai hayo hayajathibitishwa na hayajaungwa mkono na ushahidi wowote rasmi.
Kwa upande wake, FIFA haijazungumzia tuhuma hizo na imeendelea kusisitiza kuwa uteuzi wa waamuzi hufanyika kwa kuzingatia vigezo vya kitaalamu, uwezo wa waamuzi na utendaji wao katika mashindano, huku macho ya wengi yakielekezwa kwenye mchezo huo ili kuona jinsi kikosi hicho cha waamuzi kitakavyotekeleza majukumu yake.


