Klabu ya Napoli imeanza harakati za mapema kumsaka winga wa Manchester United, Jadon Sancho, kwa kufanya mawasiliano ya awali na wakala wake. Hatua hiyo inaashiria dhamira ya Napoli kutaka kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, hasa ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo anaweza kupatikana bila ada ya uhamisho mwishoni mwa msimu.

Sancho ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa, ameendelea kuvutia macho ya vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya. Ripoti zinaeleza kuwa, “vilabu vingi vinaona huu ni wakati sahihi wa kumsajili kutokana na uwezekano wa kumpata bure,” jambo linaloongeza ushindani wa saini yake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Wakati huo huo, Borussia Dortmund pia imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumrudisha nyota huyo, ambaye aliwahi kung’ara katika kikosi hicho. Hata hivyo, “kikwazo kikubwa kinabaki kuwa mshahara wake,” chanzo kimoja kikinukuliwa kikisema.
Inadaiwa kuwa Dortmund haipo tayari kulipa zaidi ya Euro 200,000 kwa wiki, kiwango ambacho kiko chini ya matarajio ya Sancho. “Mchezaji huyo anahitaji angalau Euro 200,000 kwa wiki,” huku kwa sasa akiripotiwa kulipwa takribani Euro 400,000 akiwa Manchester United.
Hali hiyo inaweka ugumu kwa baadhi ya vilabu vinavyomuhitaji, huku Napoli ikionekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi kifedha kukidhi mahitaji hayo. “Mazungumzo bado ni ya awali lakini yanaendelea vizuri,” imeelezwa katika ripoti husika.
Katika msimu huu akiwa Aston Villa, Sancho amecheza jumla ya mechi 35 katika mashindano yote, akifunga bao moja na kutoa asisti tatu. Takwimu hizo zinaonyesha bado hajarejea katika kiwango chake bora licha ya kuvutia maslahi makubwa kutoka kwa vilabu vikubwa.


