Wachezaji na wafanyikazi wa Manchester United walikumbwa na mshtuko wa tuhuma za sumu ya chakula kufuatia safari yao ya UEFA Europa League kwenda Moldova wiki iliyopita.

Kikosi cha Erik ten Hag kilicheza na Sheriff Tiraspol katika mji mkuu wa Moldova Chisinau Alhamisi usiku, na kushinda 2-0 kupitia kwa mabao ya Jadon Sancho na Cristiano Ronaldo.

 

Wachezaji wa Man Utd Imebainika Walikumbwa na Mshituko wa Sumu ya Chakula.

Kisha walirudi Manchester kwa ndege ya kibinafsi lakini baadae walianza kujisikia vibaya siku ya Ijumaa.

Kulingana na The Sun, hadi wanachama 12 katika kambi ya United waliathiriwa na wachezaji wachache walikosa mazoezi siku ya Ijumaa na wengine Jumamosi.

Ripoti hiyo inasema United wanachunguza iwapo ugonjwa huo ulitokana na chakula walichokula wakiwa Moldova au kwenye ndege ya nyumbani.

 

Wachezaji wa Man Utd Imebainika Walikumbwa na Mshituko wa Sumu ya Chakula.

United hawakucheza wikendi baada ya mchezo wa Jumapili wa nyumbani wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leeds United, kuahirishwa kwa sababu ya kiusalama kutokana na mazishi ya Malkia Elizabeth II.

Haijulikani ni jinsi gani United ingeathiriwa vibaya na ugonjwa huo ikiwa mechi ya Old Trafford isingehairishwa.

Baadhi ya wachezaji waliokosa mazoezi siku ya Ijumaa waliweza kurejea Jumamosi ,na wote walioathirika wameweza kuondoka kwa ajili ya majukumu ya kimataifa.

 

Wachezaji wa Man Utd Imebainika Walikumbwa na Mshituko wa Sumu ya Chakula.

Kuzinduka kwa United chini ya Ten Hag, ambao umewafanya kushinda michezo mitano kati ya sita iliyopita katika michuano yote, utajaribiwa baada ya mapumziko ya kimataifa watakapocheza na Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad Oktoba 2.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa