NYOTA wanne wa Simba wataukosa mchezo wa ligi kesho dhidi ya Azam kutokana na majeraha waliyonayo pamoja na kadi za njano.

Mchezo huo wa ligi utapigwa kesho alhamis kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Azam wakiwa na pointi 11 huku Simba wakiwa nazo 14.

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema “Tunamshukuru Mungu maandalizi yamekamilika mpaka hivi sasa kuelekea kwenye mchezo wetu huo wa kesho dhidi ya Azam.

“Wakati tunajiandaa kucheza na Yanga hapo pia tulijua mchezo utakaofuata ni dhidi ya Azam hivyo tulijiandaa kukabiliana nao kwani tunajua wana kikosi kizuri na kocha mzuri pia.

“Wachezaji ambao ni majeruhi ni Sadio Kanoute, Israel Mwenda, Jimmyson Mwanuke, na Mzamiru Yassin ambaye anakadi tatu za njano, lakini tayari Shomari Kapombe amerejea mazoezini na atatumika kwenye mchezo wa kesho.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa