Wayne Rooney Amuunga Mkono Michael Carrick Kuinoa Manchester United

Kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick, amesema anataka matokeo ya timu yake yawe ndiyo yanayozungumza baada ya kupewa sapoti na nguli wa klabu hiyo Wayne Rooney kuwa kocha wa kudumu wa timu hiyo. Kauli hiyo imekuja baada ya United kupata ushindi muhimu wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa Premier League uliochezwa Jumapili.

Wayne Rooney Amuunga Mkono Michael Carrick Kuinoa Manchester UnitedUshindi huo uliimarisha harakati za Manchester United kufuzu kushiriki UEFA Champions League msimu ujao. Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Casemiro, Matheus Cunha na Benjamin Sesko yaliihakikishia timu hiyo pointi tatu muhimu.

Kwa sasa Manchester United wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi tatu mbele ya Aston Villa katika mbio za kumaliza ndani ya nne bora. Ushindi huo pia ulikuwa wa saba katika mechi tisa tangu Carrick achukue majukumu ya ukocha wa muda. Matokeo hayo yameifanya United kuwa na pointi sita mbele ya Chelsea FC waliopo nafasi ya sita.

Wayne Rooney Amuunga Mkono Michael Carrick Kuinoa Manchester UnitedBaada ya mchezo huo, Rooney alimpongeza Carrick na kusema anaamini rafiki yake huyo wa zamani anastahili kupewa kazi hiyo moja kwa moja.

“Ninamfahamu Carrick vizuri sana. Najua tabia yake na namna alivyo. Timu ilihitaji mtu mwenye utulivu lakini pia anayejua klabu na wachezaji. Ameleta upendo kwa wachezaji na tunaona wanacheza kwa ubora zaidi na kwa umoja,” alisema Rooney.

Wayne Rooney Amuunga Mkono Michael Carrick Kuinoa Manchester UnitedKwa upande wake, Carrick ambaye aliwahi kuwa kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya England, alisema hataki kujishughulisha sana na mijadala kuhusu mustakabali wake.

“Kwangu hilo haliniathiri hata kidogo. Niko katika nafasi hii kwa sasa na ninajitahidi kufanya kazi yangu kadiri niwezavyo. Tunachotaka ni kuifanya timu iwe bora zaidi na kuendelea kuboresha kiwango,” alisema Carrick.

Wayne Rooney Amuunga Mkono Michael Carrick Kuinoa Manchester UnitedCarrick aliongeza kuwa ataendelea kuzingatia maendeleo ya timu huku uamuzi kuhusu mustakabali wake ukiachwa kwa uongozi wa klabu hiyo ambao unahusisha mmiliki mwenza Jim Ratcliffe.

“Tutafanya kila tuwezalo kuendelea kusonga mbele. Kitakachotokea baadaye kitatokea tu,” alisisitiza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.