Klabu ya West Ham imepanga kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kumsajiri mchezaji kutoka klabu ya Club Brugge ikiwa klabu hiyo haitapunguza ada yake ya usajiri.

Vanaken mwenye miaka 30 anamkataba na klabu ya Club Brugge mpaka 2025 na mchezaji mwenyewe anataka kwenda kucheza kwenye ligi kuu ya uingereza, Ijapokuwa Club Brugge bado hawako tayari kumruhusu kuondoka.

West Ham, West Ham Kujiondoa Kwa Vanaken, Meridianbet

West Ham tayari walishawasilisha offer mbili ambazo zote zimekataliwa kwa ajiri ya mchezaji huyo huku offer ya kwanza ikiwa na thamani ya €10milion.

West ham kwa sasa wanafikilia kumpata mbadala wa kiungo huyo mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ubelgiji, japokuwa kwa sasa wapo kwenye maongezi na klabu Club Brugge, lakini kama ada ya uhamisho haitapunguzwa basi wataachana nae.

Vanaken ameichezea Club Brugge michezo 50, huku akifanikiwa kufunga magoli 15 na kusaidia kupatikana mengine 12 kwenye mashindano yote kuanzia msimu wa 2021/22.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa