West Ham United klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza ipo kwenye mikakati mizito ya kunasa saini ya kiungo wa Olympique Lyon Lucas Pacqueta. Kiungo huyo fundi raia wa Brazil amekua akihitajika na timu kadhaa na za nchini Uingereza.

klabu ya West Ham inaendelea kufanya usajili ili kuboresha timu hiyo katika maeneo mbalimbali uwanjani ili kuifanya kua timu shindani chini ya mwalimu David Moyes.

west ham, West Ham United Yamuwinda Lucas Pacqueta., Meridianbet

West Ham ambayo ilimaliza msimu vizuri sana lakini hali imekua tofauti kwa msimu ambapo imeanza vibaya msimu huu baada ya kupoteza michezo mitatu ya kwanza ya ligi kuu Uingereza.

Wagonga nyundo hao wa London wameshamalizana na mchezaji huyo wa kibrazil kwenye maslahi binafsi changamoto imebaki kwenye klabu inayommiliki mchezaji huyo ya Olympique Lyon ambayo bado West Ham haijmalizana nayo.

Klabu ya West Ham endapo itakamilisha usajili wa Lucas Pacqueta ataungana na wachezaji kadhaa waliosajilwa dirisha hili kama Gianluca Scammaca,Maxwell Cornet, pamoja na Thilo Kehrer.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa