Waamuzi Kutoka Morocco Kuchezesha Dabi ya Kariakoo Mei 3

Dabi ya Kariakoo inayosubiriwa kwa hamu kati ya Simba SC na Yanga SC inatarajiwa kupigwa Mei 03, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, huku macho na masikio ya mashabiki yakielekezwa kwenye pambano hilo kubwa la Ligi Kuu ya NBC. Mechi hiyo imeendelea kuvuta hisia kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya timu hizi mbili kongwe nchini Tanzania.

Waamuzi Kutoka Morocco Kuchezesha Dabi ya Kariakoo Mei 3 Katika hatua ya kuhakikisha mchezo huo unachezwa kwa viwango vya juu vya haki na ubora, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwasilisha ombi rasmi kwa Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) kuomba waamuzi kutoka nchini humo kusimamia mchezo huo muhimu. Ombi hilo limekubaliwa na mamlaka husika, hatua inayotajwa kuongeza hadhi ya pambano hilo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kupitia taarifa rasmi, Shirikisho la Soka Morocco limetangaza majina ya waamuzi watakaosimamia dabi hiyo, wakiongozwa na Hamza El Faruq ambaye atakuwa mwamuzi wa kati. Uamuzi huo unaonyesha imani kubwa kwa waamuzi hao katika kusimamia michezo mikubwa ya kimataifa.

Waamuzi Kutoka Morocco Kuchezesha Dabi ya Kariakoo Mei 3 Waamuzi wengine walioteuliwa ni Lahsene Azkawi atakayekuwa msaidizi wa kwanza, Hamza El Nasri kama msaidizi wa pili, huku Mostafa Kchaaf akiteuliwa kuwa mwamuzi wa akiba (Fourth Official). Kikosi hicho cha waamuzi kinatarajiwa kuwasili nchini kabla ya siku ya mchezo kwa maandalizi ya mwisho.

Waamuzi Kutoka Morocco Kuchezesha Dabi ya Kariakoo Mei 3 Uteuzi wa waamuzi wa kimataifa kutoka Morocco unatazamwa kuongeza uwazi na kuondoa malalamiko ya upendeleo ambayo mara nyingi huibuka kwenye michezo mikubwa kama hii. Mashabiki wa soka nchini sasa wanasubiri kwa hamu kuona nani ataibuka mshindi katika dabi hiyo yenye historia na mvuto mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.