Xabi Alonso Apewa Nafasi Kubwa Kuinoa Chelsea Msimu Ujao

Klabu ya Chelsea inaendelea kufanya mazungumzo ya awali ili kufahamu kiwango cha utayari wa kocha Xabi Alonso kujiunga na timu hiyo kama kocha mkuu mpya kuelekea msimu ujao. Ripoti zinaeleza kuwa Chelsea wanamtazama Alonso kama chaguo lao kuu katika mpango wa kuijenga upya timu na kurejesha matumaini ya mashabiki wa klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Xabi Alonso Apewa Nafasi Kubwa Kuinoa Chelsea Msimu UjaoVyanzo vya karibu na klabu hiyo vinaeleza kuwa Alonso ameonyesha kuwa na mtazamo chanya kuhusu nafasi hiyo, lakini moja ya mambo anayoyapa kipaumbele ni kupata uhakika wa kiwango cha mamlaka na ushawishi atakaokuwa nao ndani ya klabu. “Alonso anataka kujua atakuwa na nafasi gani katika maamuzi muhimu ya timu kabla hajafanya uamuzi wake wa mwisho,” kilieleza chanzo hicho.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mbali na Alonso, Chelsea pia wanamfikiria Cesc Fabregas kama mmoja wa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuinoa timu hiyo. Hata hivyo, viongozi wa klabu wanaonekana kuweka nguvu zaidi kwa Alonso huku wakiamini anaweza kuleta utambulisho mpya na mfumo imara wa uchezaji ndani ya kikosi hicho.

Xabi Alonso Apewa Nafasi Kubwa Kuinoa Chelsea Msimu UjaoMchakato wa kutafuta kocha mpya unasimamiwa na wakurugenzi wa michezo Paul Winstanley pamoja na Laurence Stewart, kipindi ambacho mashabiki wa Chelsea wameendelea kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa timu pamoja na mfumo wa uendeshaji wa klabu. Hali hiyo imeongeza presha kwa uongozi kufuatia matokeo mabaya ya mwishoni mwa msimu.

Xabi Alonso Apewa Nafasi Kubwa Kuinoa Chelsea Msimu UjaoTaarifa zinaeleza kuwa Chelsea wanataka kuhakikisha wanampata kocha mpya kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia. Aidha, klabu hiyo ina wasiwasi kuwa kushindwa kufuzu michuano ya Ulaya kunaweza kuathiri uwezo wao wa kuvutia wachezaji wakubwa katika dirisha lijalo la usajili, jambo ambalo limeifanya klabu hiyo kufikiria pia kusajili wachezaji wenye uzoefu zaidi.

Xabi Alonso Apewa Nafasi Kubwa Kuinoa Chelsea Msimu UjaoWakati maamuzi kuhusu benchi la ufundi yakiendelea kusubiriwa, Chelsea bado wana nafasi ya kurejesha sehemu ya heshima yao msimu huu watakapocheza dhidi ya Manchester City kwenye fainali ya Kombe la FA itakayopigwa mwishoni mwa wiki katika dimba la Wembley.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.