Xabi Alonso ataka Chelsea ijenge njaa ya ushindi

Kocha mpya wa Chelsea, Xabi Alonso, amesema anataka kuijenga timu yenye njaa kubwa ya mafanikio baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuinoa klabu hiyo ya Stamford Bridge. Alonso amesisitiza kuwa lengo lake ni kurejesha ari ya ushindani na mafanikio ndani ya kikosi hicho.

Xabi Alonso ataka Chelsea ijenge njaa ya ushindiAkizungumza katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari, Alonso alisema kurejea kwenye mashindano ya Ulaya ni moja ya malengo makuu ya Chelsea, lakini hilo litahitaji juhudi za pamoja. “Bila shaka hilo ni lengo letu, lakini ili kulifikia tunapaswa kufanya mambo mengi kwa usahihi. Tunahitaji kujua tunataka kuchezaje, tunataka kujionaje na namna tunavyotaka kuikabili kila mechi,” alisema.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 alieleza kuwa bado yupo katika hatua za mwanzo za kuijenga timu na anasubiri kuwa na kikosi kamili kabla ya kufanya tathmini ya mwisho. “Hii ndiyo kazi yangu na ninatarajia kwa hamu kuwa na wachezaji wote pamoja. Kwa sasa bado ni siku za mwanzo na baadhi ya masuala yanaendelea,” aliongeza.

Xabi Alonso ataka Chelsea ijenge njaa ya ushindiMbali na kuzungumzia Chelsea, Alonso pia alitoa maoni yake kuhusu michuano ya Dunia linaloendelea na kukumbuka mafanikio yake akiwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2010. Hata hivyo, alikwepa kuweka malengo mahususi ya msimu wake wa kwanza akiwa Stamford Bridge.

Xabi Alonso ataka Chelsea ijenge njaa ya ushindiAkihitimisha, Alonso alisisitiza kuwa mafanikio yatategemea mtazamo wa kila mtu ndani ya klabu. “Sisi Chelsea tunapaswa kushirikiana nguvu, kuwa na malengo makubwa na zaidi ya yote kuwa na njaa ya kutaka kushinda. Huo ndio msingi wa mafanikio tunayoyahitaji,” alisema.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.