Xavi Hernandez kocha wa klabu ya Fc Barcelona amewatakamwachezaji wake kuonesha uwezo ili kuweza kupata matokeo katika mchezo ikiwa ni katika utawala wake Barca ikishinda itakua inashinda baada ya muda mrefu.

Barca wameshinda mara mbili tu dhidi ya Fc Bayern katika mechi 13 za mwisho walizokutana na wababe hao wa Ujerumani na hawajawahi kushinda mchezo wa ugenini dhidi ya timu hiyo.

xaviBlaugrana wamefungwa mechi nane kati ya kumi na moja walizocheza na Bayern munich,Barca waliangukia kipigo cha aibu mwaka 2020 kwa jumla ya 8-2 kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya mchezo uliopigwa pale Lisbon.

Klabu hiyo ambayo inaonekana kuimarika sana tangu kuchukuliwa na kiungo gwiji wa klabu hiyo Xavi Hernandez mwezi wa kumi na oja mwaka jana.

Xavi anaeleza”Tunajua watu wengi wameweka matarajio makubwa kwetu msimu huu lakini nafikiri kushinda mchezo wetu wa jumanne ni muhimu zaidi kwasababu tunajua hii ni sehemu ambayo hatukuwahi kushinda pia”

“Tumefanya kazi kwa miezi kumi,nafikiri tumekua na tunahisia tunaweza kushinda mchezo huu na kuonesha kuna kitu kimebadilika”.

“Tunakwenda kucheza na timu bora kabisa ulimwenguni hivo tukishinda mchezo huo itaonesha namna gani tumebadilika kama timu”aliongeza pia Xavi kwa kusema mchezo huo unalama tatu tu muhimu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa