Xhavi Hernandez ambaye ni kocha mkuu wa Barcelona amesema  kuwa “Maisha yapo juu ya Soka” baada ya mechi kati ya timu yake na Cadiz kusimamishwa kwa muda kutokana na shabiki wake kusumbuliwa na mshtuko wa moyo.

 

Xhavi: "Maisha ya Binadamu na Soka"

Wageni ambao ni Barcelona walikuwa wamefunga mabao mawili zikiwa zimesalia dakika tisa kumalizika kwa mchezo huo, ndipo ukasimamishwa na wachezaji kutolewa uwanjani kwasababu ya dharura ya kiafya.

Mlinda mlango wa Cadiz Jeremia Ledesma alionekana akipitisha kifaa cha matibabu kabla ya wachezaji husika kushuka kwenye  mtaro, na baadae Cadiz walitoa taarifa kuthibiisha kuwa shabiki huyo alikuwa ametulia na kupelekwa katika hospitali ya karibu Puerta Del Mar. Opareta wa kamera alizirai pia katika tukio tofauti na alitibiwa haraka na wafanyakazi wa uwanja huo.

Xhavi: "Maisha ya Binadamu na Soka"

Mara baada ya mchezo kuanza tena baada ya kuchelewa kwa dakika 40, vijana wa Xhavi waliongeza mabao kutoka kwa Frank De Jong na Robert Lewandowski kupitia kwa Ansu Fati na Ousmane  Dembele na kumalizika kwa Barca kushinda kwa mabao 4-0.

 

Xhavi: "Maisha ya Binadamu na Soka"

Xhavi alifurahi kutokana na timu yake kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo lakini pia akasema maisha ya binadamu yapo juu ya soka,

“Kwa bahati nzuri, hakuna bahati mbaya iliyotokea na tumeweza kucheza mpira” “Mwishowe lilikuwa ni suala la ubinadamu, huku sifa za ubinadamu zikitoka kati yetu sote, tumejaribu kuongeza na tunatumai itakuwa vyema kwa mtu anayehusika”

Ushindi wa Barca kwao ulikuwa wa kwanza dhidi ya Cadiz katika majaribio matano, wakiwa wametoka sare mbili, na kupoteza mechi mbili kati ya nne katika msururu wa nyuma toka April 2006. Barcelona sasa wameshinda mechi nne na kutoka sare moja kati ya mechi tano za kwanza za Laliga walizocheza.

 

Xhavi: "Maisha ya Binadamu na Soka"

Mechi yao inayokuja itakuwa ni ya michuano ya klabu bingwa dhidi ya Bayern Munich ambapo mara ya mwisho kukutana Xhavi alipoteza michezo yote, wanakutana huku kila mmoja akiwa ameshinda mechi ya kwanza ambapo Bayern alishinda dhidi ya Inter huku Barca akishinda dhidi ya Viktoria Plizen.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa