Yamal: Mechi dhidi ya Ufaransa ndiyo muhimu zaidi kuwahi kuicheza

Nyota wa Hispania, Lamine Yamal, amesema nusu fainali ya michuano ya Dunia dhidi ya Ufaransa ndiyo mechi muhimu zaidi kuwahi kuicheza katika maisha yake ya soka.

Yamal: Mechi dhidi ya Ufaransa ndiyo muhimu zaidi kuwahi kuichezaWinga huyo wa Barcelona amesema licha ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na mdogo wake kuteka mitandao ya kijamii, akili yake yote ipo kwenye pambano hilo kubwa, akisisitiza kuwa anaishi ndoto ya kucheza mechi ya hadhi hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Yamal amesema hana hofu yoyote ya kuikabili Ufaransa na kufafanua kauli yake iliyozua mjadala kuhusu wapinzani wao. “Waliniuliza kama ninaogopa Ufaransa, nikasema hapana. Sisi ni mabingwa wa Ulaya. Ni mpira wa miguu tu, hakuna kingine,” alisema. Pia alieleza kuwa hana presha kabla ya mchezo huo, akiongeza: “Niko mtulivu sana. Nitacheza kwa namna ninavyojua, na ukitoa kila kitu uwanjani, hakuna sababu ya kuwa na presha.”

Yamal: Mechi dhidi ya Ufaransa ndiyo muhimu zaidi kuwahi kuichezaAkizungumzia umuhimu wa mchezo huo, Yamal alisema unazidi hata fainali ya Euro au mechi yoyote ya Ligi ya Mabingwa aliyowahi kucheza akiwa Barcelona. “Hii ndiyo mechi namba moja kwangu. Bila shaka ndiyo muhimu zaidi nitakayowahi kuicheza,” alisema. Pia alionyesha imani kubwa kwa kikosi cha Hispania, akisema: “Ndiyo, tunaamini tutakuwa mabingwa. Ni safari ngumu, lakini kwa nini isiwe kama mwaka 2010?”

Yamal: Mechi dhidi ya Ufaransa ndiyo muhimu zaidi kuwahi kuichezaKuhusu rekodi yake ya kufunga bao moja pekee kwenye mashindano hayo, Yamal amesema hilo halimsumbui. “Kila mashindano ni tofauti. Si kosa la kocha kwamba sijafunga mabao matano. Muhimu ni kwamba tunashinda. Natumaini kwenye mechi ijayo nitafunga,” alisema. Pia alisisitiza kuwa mpira wa miguu unapaswa kuunganisha watu badala ya kuibua migawanyiko.

Yamal: Mechi dhidi ya Ufaransa ndiyo muhimu zaidi kuwahi kuichezaAkihitimisha mazungumzo yake na waandishi wa habari, Yamal alitania kuhusu maoni yanayotolewa dhidi yake. Tangu Euro tumekuwa tukikua kama timu. Mnasema sipo kwenye kiwango changu bora, hivyo msitarajie makubwa kutoka kwangu. Lakini naamini itakuwa siku nzuri,” alisema kwa kujiamini huku akielekea kwenye pambano linalosubiriwa kwa hamu dhidi ya Ufaransa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.